pmbet

Dulla Makabila amuomba msamaha Majizzo

Sisti Herman

June 26, 2024
Share :

Ikiwa imepita wiki chache tangu msanii maarufu wa Singeli nchini Dulla Makabila 'kuponda' hadharani matukio yaliyoambatana na uandaaji wa moja kati ya matamasha yanayoandaliwa na mmilikiwa EFM & TVE Francis Ciza 'Majizzo' kuhusu namna wasanii wa muziki wa Singeli wanavyofanyiwa. msanii huyo leo ameomba radhi hadharani na kukiri kuwa namna ya ufikishaji wa ujumbe wake haukuwa sahihi.

Ameandika Dulla Makabila kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram;
______

BABA ANGU LEO NIMEWAZA KIUPANA NIMEGUNDUA NIMEKUKOSEA SANA MANENO NILIYOANDIKA MTANDAONI MIEZI KADHAA NYUMA KUHUSIANA NA WEWE YALILETA TAFSIRI YA UTOVU WA NIDHAMU KWAKO NA KWA TAASISI NZIMA NA WAFANYA KAZI KWA UJUMLA KIUKWELI NAJIONA MKOSEFU SANA TENA SANA HASA KWAKO MTU AMBAE ULIONA KIPAJI CHANGU NA UKANITOA NYUMBANI KWETU KUTOKA KWENYE KULALA CHUMBA KIMOJA NA DADA ZANGU NA KUNIPANGIA NYUMBA NA KUNIFANYIA PROMO USIKU NA MCHANA MPAKA MUNGU ALIPOJAALIA NIKAWA STAR KWENYE HUU ULIMWENGU TENA ULIJITOLEA KUNISAIDIA BILA MKATABA WALA KUTAKA MASLAHI YEYOTE KUTOKA KWANGU KIUKWELI NIMEKOSEA SANA NAOMBA UNISAMEHE MZEE WANGU MIMI NI MTOTO WAKO NA SIDHANI KAMA NI UJINGA KWA MTOTO KUMUANGUKIA BABA AKE ANAPOKOSEA MAANA NAAMINI MAKOSA TUMEUMBIWA BINADAMU NA KUKOSEA NDIO KUJIFUNZA MZEE WANGU NAOMBA UNISAMEHE SANA BUSARA ZAKO NA MAARIFA YAKO BADO NAVIHITAJI SANA KWENYE SAFARI YANGU NA NAJUA PAMOJA NAKUKOSEA KOTE NAKOKUKOSEAGA HAUJAWAHI KUFURAHIA ANGUKO LANGU NDOMANA KIPO KIPINDI NILIKUA NADHANI KWA VILE HATUPO SAWA BASI UTAKUA NA CHUKI NA MIMI KUMBE ATA SHOW NILIZOKUA NAFANYA WEWE NDIO ULIKUA UNAPITISHA JINA LANGU BILA MIMI KUJUA NA ATA WEWE WALA HAUKUTAKA NIJUE MZEE NAOMBA UNISAMEHE SANA WEWE NDIO BABA ANGU NA WEWE NDIO MLEZI WANGU NA SIO TU WEWE ATA NDUGU ZANGU WOTE NILOWAKOSEA NAOMBA MNISAMEHE @samio_love NAOMBA UNISAMEHE πŸ™πŸΎ@meneja_kandoro NAOMBA UNISAMEHE @ashamangatz NAOMBA UNISAMEHE πŸ™πŸΎ @bigdady_dizzo NAOMBA UNISAMEHE @sseboefm NAOMBA UNISAMEHE πŸ™πŸΎ @hermyb NAOMBA UNISAMEHE SANA NA WAFANYA KAZI WOTE WA @efmtanzania NA MASHABIKI ZANGU AMBAO HAMKUPENDEZWA NA KILICHOTOKEA NAOMBA MNISAMEHE PIAπŸ™πŸΎπŸ™πŸΎπŸ˜­πŸ˜­

NAWAAHIDI KUWA SWALA KAMA HILI HALITAJIRUDIA TENA KWENYE MAISHA YANGU YA MZIKI πŸ™πŸΎπŸ™πŸΎπŸ™πŸΎπŸ™πŸΎ
____

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet