Dulla Makabila amuwashia moto Majizzo
Joyce Shedrack
April 27, 2024
Share :
Msanii wa muziki wa Singeli, Dulla Makabila ameibuka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram akiandika ujumbe mrefu na kumpiga mkwara mmiliki wa EFM na ETV, Majizzo baada ya kushindwa kupanda jukwaani kutumbuiza kwenye hafla ya kusherekea kutimiza miaka kumi ya EFM na TVE iliyofanyika usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa.
Dulla Makabila ameandika ujumbe huo akiwashutumu watu waliokuwa na mamlaka ya kuwapandisha wasanii jukwaani kutokumpandisha yeye kwa wakati yaani muda wa saa 4 aliopangiwa na kusubiri hadi saa 11 alfajiri ambapo pia alishindwa ku-perfom.
"Mzee watu wako uliowapa mamlaka ya kusisamia baadhi ya shughuli hasa za show wana wasanii wao wanaowapenda na kiukweli hao wasanii hawajafika bado sehemu ambayo sisi wengine tumefika ila kwa vile wana uwezo wa kuwa control basi wanawapa nafasi kubwa na kutudidimiza sisi ambao hawana uwezo wa kutubania ata mia yetu kwenye hela ya show kutokana na connection zetu na namna ambayo tuna uwezo ata wa kupiga simu na kuambiwa kiasi ambacho kilichotolewa kwenye show sasa iyo ndo sababu iliyofanya tuchukiwe jana nimefika kwenye show ilikuwa nipande saa 4 ila sikupandishwa mpaka saa 11 alfajiri ndo wanataka nipande tena aliyepewa ratiba ety kaenda kujificha ili tusiende kumfata na akawa anapandisha watu wake anaowataka yeye kiukweli niliumia nilipofikilia shabiki yangu aliyekuwa ananisubiri uku ananyeshewa na mvua kuanzia saa 10 jioni hadi saa 11 alfajiri na bado ameondoka bila mimi kupanda jukwaani"
Hayo ni baadhi ya maneno aliyoandika Makabila akionekana kuumizwa na kitendo cha yeye kushindwa ku-perfom kwenye show hiyo.
Waraka huo haukuishia hapo Dulla alimpiga mkwara Majizzo akisema kuanzia sasa hataki kushiriki kwenye kazi yoyote aliyoiandaa Majizzo.
"Sasa kuanzia leo mzee wangu si wanasemaga siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa sasa mimi baba angu sio ao mbwa wako tu ata wewe sitaki kuongea na wewe wala sitaki unishilikishe tena jambo lako lolote"
Makabila amemaliza kwa kuandika ipo siku wasanii wa singeli tutapata media itakayoheshimu mziki wetu kama wanavyofanya kwa miziki mingine.