Dulla Makabila anaponzwa wanawake - Lavalava (VIDEO)
Eric Buyanza
December 6, 2023
Share :
Msanii wa kizazi kipya Abdul Juma Iddi "Lavalava" amethibitisha kutarajia kufunga mwaka na nyimbo moja kali huku akithibitisha kuwa kati ya wasanii aliofanya nao ngoma ni pamoja na Billnass.
"Nina nyimbo kali sana na Billnass ya kufunga mwaka, huwa sitoi nyimbo mara kwa mara ila nikitoa lazima iwe Hit" alijigamba Lavalava kwenye mahojiano maalum na PMTV.
Pia msanii huyo ametoa maoni yake kuhusu watu wanaosema yeye hana nyota na hata baadhi ya wasanii wenzake kusema kuwa analogwa na wenzake
"Watanzania waache kugawa riziki kwenye midomo, namwachia Mungu, binafsi naishi vizuri sana, huyo Dulla Makabila anayesema nalogwa anaponzwa sana na wanawake hadi wanamharibu kisaikolojia" alimaliza Lavalava.