EAC Yatoa tahdhari ya homa ya nyani
Sisti Herman
July 31, 2024
Share :
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) juzi Jumatatu Julai 29 2024 ilitoa wito kwa nchi nane wanachama wake kutoa elimu kwa raia wao jinsi ya kujikinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa homa ya nyani (monkeypox), unaoambukiza.
Tahadhari hiyo inafuatia ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), zote wanachama wa EAC, zinakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa huo.
EAC ilisema katika taarifa yake iliyotolewa kutoka makao makuu yake. jijini Arusha ilisema, Burundi imethibitisha visa vitatu katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo, vilivyothibitishwa na maabara za kitaifa na WHO. Tangu 2022, DRC imeripoti zaidi ya kesi 21,000 za mpox na zaidi ya vifo 1,000, kulingana na WHO.
Burundi inapakana na DRC, Rwanda na Tanzania, wakati DRC inapakana na nchi tano wanachama wa EAC - Tanzania, Burundi, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini. Kenya na Somalia pia ni wanachama wa EAC.
“Nchi wanachama wa EAC lazima zitoe taarifa muhimu kuhusu ugonjwa huo na kuchukua hatua za kujikinga,” Andrea Aguer Ariik Malueth, Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia sekta ya miundombinu, uzalishaji, kijamii na kisiasa
Virusi vya m-pox huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu na huenea kati ya watu kupitia mawasiliano ya karibu, vitu vilivyoambukizwa na matone yanayotokana na kupumua.
Dalili za ugonjwa wa mpoksi ni pamoja na upele au vidonda kwenye ngozi, homa, maumivu makali ya kichwa, maumivu ya misuli, maumivu ya mgongo, udhaifu wa jumla wa mwili na nodi za limfu kuvimba, kwa kawaida huchukua wiki mbili hadi nne.
Ingawa kesi nyingi ni ndogo, kesi kali na vifo vinaweza kutokea, taarifa hiyo ilisema.