Ebola yakatisha safari ya Simba Kenya
Sisti Herman
November 12, 2026
Share :

Simba SC imeamua kusitisha mpango wa kuweka kambi maalum nchini Kenya kwa ajili ya kujiandaa na mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na hofu ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.
Sababu nyingine ni masharti ya Morocco kwa wasafiri wanaotoka Kenya, DR Congo na Uganda, ambapo wanatakiwa kuwa wametimiza siku 30 tangu kuondoka katika nchi hizo kabla ya kuruhusiwa kuingia nchini humo.
Simba inahofia kwenda Kenya kwa sasa kunaweza kuikwamisha kusafiri kwenda Morocco kwa ajili ya kucheza dhidi ya RS Berkane katika mechi ya pili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inayotarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 18 na 20, 2026.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema klabu hiyo inaendelea kufanya tathmini na itatoa taarifa rasmi ndani ya siku mbili kuhusu hatma ya safari hiyo.
Awali, Simba ilipanga kwenda Kenya baada ya kualikwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia Novemba 15, 2026, katika kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.
Hata hivyo, Simba imekuwa na mwenendo mzuri msimu huu, ikiwa imeshinda mechi zote 10 za Ligi Kuu Tanzania Bara na kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.





