Eddie Murphy afunga ndoa baada ya uchumba uliodumu kwa miaka 6
Eric Buyanza
July 13, 2024
Share :
Nyota wa movie ya 'Coming to America', Eddie Murphy amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu mwanamitindo Paige Butcher.
Wanandoa hao waliokuwa kwenye uchumba kwa takriban miaka miaka sita, walifunga ndoa katika sherehe ya faragha iliyojumuisha familia na marafiki wachache wa karibu.
Harusi ya wawili hawa ilfanyika huko Anguilla kwenye visiwa vya Caribbean.
Eddie Murphy ana miaka 66 na mke wake mwanamitindo wa Australia, Paige Butcher, ana umri wa miaka 44.