pmbet

Edin Terzic na safari ya Kutoka kuwa Shabiki hadi Kuwa Kocha Dortmund

Sisti Herman

May 8, 2024
Share :

'Maisha yanaenda kasi sana' 

Je ulishawahi kuusikia huu msemo? kama hujawahi basi umetimia kwa kocha wa Borrusia Dortmund Edin Terzic ambaye jana ameiwezesha timu hiyo kutinga fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwanyuka PSG na kuwaondoa kwenye nusu fainali ya kichuano hiyo kwa jumla ya magoli 2-0, nyumbani na ugenini.

Miaka 12 iliyopita kocha huyo alikuwa mmoja wa mashabiki waliokuwa wameketi jukwaani wakati kocha Jurgen Klopp akiwapa taji la Bundesliga mwaka 2012.

Baada ya mwaka huo Edin alianza kama msaka vipaji wa klabu hiyo mwaka 2010 kabla ya baadae kuwa kocha msaidizi na baadae kuwa kocha mkuu wa timu za vijana wa klabu hiyo.

Edin aliondoka kwenye timu hiyo kwenda West Ham na Besiktas kwa nyakati tofauti kuwa kocha msaidizi na kupata uzoefu kabla ya kurejea Dortmund mwaka 2018.

Baada ya kurejea Dortmund Edin alianza kuwa kama Kocha muda na baadae kuwa Mkurugenzi wa ufundi na sasa kocha Mkuu.

Mei 28 kwenye dimba la Wembley atakabiliana mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Real Madrid na Bayern itakayopigwa leo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet