Ekari 291 za bangi zateketezwa wilaya za Tarime na Rorya
Eric Buyanza
July 25, 2026
Share :

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema Mkoa wa Mara umefikia mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya kilimo cha bangi, ambapo kiwango cha uzalishaji kimepungua kwa takribani asilimia 80 kutokana na operesheni endelevu zinazotekelezwa na Serikali.
Katika operesheni maalumu zilizofanyika Wilaya za Tarime na Rorya, DCEA iliteketeza ekari 291.2 za mashamba ya bangi, ilikamata magunia 15 ya bangi kavu na pikipiki nne zilizokuwa zikitumika katika shughuli haramu.
Wananchi wameendelea kuhamasishwa kuachana na kilimo cha bangi na kujikita katika shughuli halali za uzalishaji kwa maendeleo ya familia na Taifa.





