El Clasico, Madrid na Barca kuumana Jumapili
Sisti Herman
April 18, 2024
Share :
Jumapili hii ya Aprili 21 ligi kuu Hispania itashuhudia mchozo mkubwa zaidi wa ligi hiyo kati ya Real Madrid watakaowakaribisha Barcelona kwenye dimba lao la nyumbani Santiago Bernabeu.
Kwa misimu ya karibuni mechi hio yenye utani wa jadi imepungukiwa na hamasa baada ya kuondoka kwa wachezaji nyota wa timu hizo ambao pia ni washindi wa tuzo za Ballon D'or Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
Kwasasa wachezaji wenye kiwango bora zaidi kwenye vilabu hivyo ni Jude Bellingham wa Real madrid mwenye magoli 16 na asisti 4 lakini pia Robert Lewandowski wa Barcelona mwenye magoli 13 na asisti 9.
Hadi sasa kwenye msimamo wa ligi Real Madrid wanaongoza wakiwa na alama 78 wakifuatiwa na Barca wenye alama 70 wote wakiwa wamecheza mechi 31.
Je nani kuibuka mshindi.