EL Clasico nje ya uwanja penzi la Lamine lavunjika kisa nyota wa Madrid.
Joyce Shedrack
September 4, 2025
Share :
Penzi kati ya nyota wa Barcelona Lamine Yamal na Mwanamuziki wa Argentina Nicki Nicole limevunjika rasmi ikiwa ni siku 13 tu tangu wajitambulishe kuwa pamoja kupitia mitandao yao ya kijamii.

Ripoti kutoka Hispania zinaeleza kuwa chanzo cha wawili hao kutengana ni kutokana na mrembo huyo kugundulika kuwa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na mchezaji wa Real Madrid Franco Mastantuono.
Agosti 25 Lamine alimzawadia Nicole gari mpya aina ya Ferrari SF90 na kuachia picha zao za pamoja kwenye Mitandao Ya kijamii kwa kuthibitishia Umma kuwa wao ni wapenzi licha ya kupishana miaka 7.