pmbet

El Nino yabadili ratiba za mitihani ya Taifa

Sisti Herman

September 25, 2026
Share :

 

Kutokana na tahadhari ya mvua za El Nino Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limefanya marekebisho ratiba ya mitihani ya kitaifa na upimaji iliyotakiwa kufanyika Oktoba na Novemba mwaka huu.

Akizungumza leo Ijumaa Septemba 25, 2026 Naibu Waziri wa Elimu, Wanu Hafidh Ameir amesema uamuzi huo umefanyika ili kuhakikisha usalama wa mitihani hiyo, wanafunzi na wasimamizi.

Amesema pamoja na taarifa zilizopokewa kutoka katika mikoa kuhusu maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo, wizara imeona kuna umuhimu wa kufanya marekebisho ya ratiba ya uendeshaji wa Upimaji na Mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026.

“Lengo la marekebisho ya ratiba ni kuhakıkisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na maofisa wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kulinda mitihani, vifaa na nyaraka za mitihani. Iwapo mvua kubwa zitatokea mwezi Novemba 2026,” amesema.

Kwa mujibu Katibu Mtendaji wa Necta, Profesa Said Mohamed, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 5 na 6 badala ya Oktoba 21 na 22, huku Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili uliopaswa kufanyika Novemba 17 na 18 sasa utafanyika Oktoba 7 na 8.

Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili uliopaswa kufanyika Novemba 2 hadi 13 sasa utafanyika kuanzia Oktoba 12 hadi 23 wakati Mtihani wa Kidato cha Nne ilioapaswa kuanza Novemba 9 hadi 27 sasa utaanza Oktoba 19 na kumalizika Novemba 6, 2026.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet