'Electric Eel', samaki mwenye uwezo wa kutengeneza umeme mpaka Volt 500
Eric Buyanza
May 21, 2024
Share :
Samaki anayejulikana kwa jina la kingereza 'Electric Eel' anayepatikana katika mto wa Amazon Barani Amerika Kusini, ni moja ya samaki wenye uwezo wa kuzalisha nguvu ya umeme kwa mwili wake.
Samaki huyo ana uwezo wa kuzalisha nguvu ya umeme inayofikia Volt 500 ikiwa ni mara mbili ya umeme wa majumbani ambao ni Volt 240.
Umeme unaozalishwa na Samaki huyo unaweza kuua viumbe mbalimbali kama binadamu na hata mamba.
Samaki huyo hutumia nguvu hiyo kama silaha yake ya kujilinda dhidi ya maadui na vilevile kujipatia chakula kama samaki wenzake na wadudu wengine wa majini.