pmbet

Elias atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka Bibi kizee

Eric Buyanza

May 23, 2024
Share :

Mahakama ya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoa wa Njombe imemhukumu Elias Thomas Mwanzalila (miaka 30) mkazi wa Mtaa wa Igima kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka Bibi kizee wa miaka 81.

Thomas alitenda kosa hilo Februari 19,2024 huko Wanging’ombe Mkoa wa Njombe.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu, Jaji Jamsi Emmanuel Mhone amesema Mahakama imejiridhisha kwa ushahidi uliotolewa na kumkuta mtuhumiwa na hatia hiyo ya ubakaji.

Hivyo, Mahakama imemhukumu miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo vya ukatili. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet