pmbet

Elimu ya ufundi ni mkombozi wa Ajira - Kinana

Eric Buyanza

December 26, 2023
Share :

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amezihimiza taasisi za kijamii kuweka mkazo katika elimu ya ufundi na ujasiriamali, ili kupata mwarobaini wa tatizo la ajira na kuzalisha wataalamu wengi zaidi wa fani mbalimbali.
 

Kinana ameyasema jijini Arusha, alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 10 wa Jukwaa la Vijana wa Kiislamu Mkoa wa Arusha (JUVIKIBA).
 

Amesema, endapo taasisi za kijamii zitajikita kuhamasisha elimu ya ufundi, vijana wengi watapata utaalam katika fani mbalimbali ambao utawawezesha kujiajiri, kuajiri wenzao na hata kuwa na sifa ya kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ya fani walizozisomea badala ya kusubiri ajira kutoka serikalini.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet