pmbet

Elneny athibitisha kuondoka Arsenal kwa ujumbe mzito

Eric Buyanza

May 18, 2024
Share :

Mohamed Elneny, mchezaji wa muda mrefu zaidi wa Arsenal, amethibitisha kwamba ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa takriban miaka nane na nusu.

Kiungo huyo wa kati wa Misri, mwenye umri wa miaka 31, amekuwa kaskazini mwa London tangu mwaka 2016 lakini atawaaga rasmi 'The Gunners' mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Elneny alisajiliwa kipindi cha Arsene Wenger akitokea FC Basel ya Uswizi kwa ada ya pauni milioni 5 na ameichezea klabu hiyo mechi 161.

Akizungumza jana kwenye video aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii Elneny alisema: "Gooners, niko hapa leo kuwatumia ujumbe, kuwaaga na kuwashukuru kwa yote mliyonifanyia....kwa kweli nitawakumbuka sana na mtabaki moyoni mwangu milele”.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet