Elon Musk aangushwa, sasa tajiri namba 1 duniani ni Jeff Bezos
Eric Buyanza
March 5, 2024
Share :
Baada ya kukaa kileleni kwa zaidi ya miezi tisa, Elon Musk amevuliwa taji la kuwa mtu tajiri zaidi duniani.
Elon Musk amepoteza taji hilo kwa Jeff Bezos baada ya hisa katika kampuni yake ya Tesla kushuka kwa 7.2% siku ya Jumatatu.
Musk sasa ana utajiri wa dola bilioni 197.7 huku utajiri wa Bezos ukiwa dola bilioni 200.3