Eminem amerudi, kuachia albam yake ya 12
Eric Buyanza
April 27, 2024
Share :
Rapa mkongwe Eminem ametangaza kuwa ataingiza sokoni albam yake ya kumi na mbili iitwayo 'The Death of Slim Shady (Coup de Grâce)' ifikipo msimu wa majira ya joto.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 51 hivi sasa, alithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema jana kwa kutupia kionjo kifupi cha video.