pmbet

Endrick aaga Brazil kujiunga na Madrid

Sisti Herman

May 31, 2024
Share :

Kinda mpya wa Real Madrid Endrick Felipe Moreira da Sousa, raia wa Brazil alitokwa na machozi wakati akiwaaga mashabiki wa klabu iliyomlea tangu akiwa na miaka 10.

Endrick mwenye miaka 17 amewaaga Palmeiras jana kwenye Mchezo wake wa mwisho kuitumikia klabu hiyo mwezi July mwaka huu 2024 atajiunga rasmi na klabu ya Real Madrid.

Kinda huyo alifunga magoli mawili akiwa na timu ya Taifa ya Brazil, kwenye michezo miwili ya kimaitaifa dhidi ya Hispania na Uingereza kwenye viwanja vikubwa duniani, Wembley na Santiago Bernabeu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet