Endrick acheza mchezo wake wa kwanza Madrid wakichapwa na AC Milan
Sisti Herman
August 1, 2024
Share :
Kinda mpya wa Real Madrid ya Hispania raia wa Brazil Endrick jana amecheza mchezo wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo kwenye mechi za maandalizi ya msimu mpya dhidi ya klabu ya AC Milan ya Italia ambapo Madrid ilipoteza 1-0.
Madrid watacheza dhidi ya Barcelona siku ya jumapili kwenye dimba la Metlife stadium East Rutherford nchini humo wakiendelea na michezo ya maandalizi ya msimu mpya kisha Milan watavaana na Barcelona siku 3 baadae.