pmbet

Endrick atambulishwa baba yake amwaga machozi jukwaani.

Joyce Shedrack

July 27, 2024
Share :

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Brazil Endrick Felipe Moreira De Sousa mwenye umri wa miaka 16 ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu akitokea katika klabu ya Palmeiras ya nyumbani kwao Brazil.

 

Mchezaji huyo ambaye amekabidhiwa jezi namba 16 alisema tangu akiwa mtoto alikuwa shabiki wa Real Madrid na leo anafuraha kuwa mchezaji wa klabu hiyo kubwa Duniani.

 

Utambulisho wa mchezaji huyo ulihudhuriwa na mashabiki wa Madrid,mashabiki wa Timu ya Taifa ya Brazil ,familia yake pamoja na wachezaji wa zamani wa klabu ya Madrid.

Wakati wa utambulisho,Baba yake mzazi Douglas de Sousa Silva Ramos alionekana akilia kwa hisia kali  pale tu alipomuona mtoto wake akivaa jezi ya Madrid kwa mara ya kwanza katika maisha yake..

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet