Endrick hakamatiki Brazil, atupia tena dhidi ya Mexico
Sisti Herman
June 9, 2024
Share :
Baada ya kuzifunga timu mbli kubwa barani Ulaya, Uingereza na Uhispania kwenye viwanja vikubwa Wembley na Santiago Bernabeu, kinda wa Brazil Endrick ameendelea kuwa na mwendelezo kwenye timu ya taifa mara baada ya kufunga goli la tatu kwenye mechi tatu mfululizo dhidi ya Mexico, Brazil wakishinda 3-2.
Endrick ambaye amekuwa hapati dakika 90 kwasababu ya kuzidiwa uzoefu na uwezo na wachezaji wenzake lakini kadiri muda unavyozidi kwenda ameendelea kutupia nyavuni na kuendelea kupata uzoefu.
Kwenye mchezo huo ambao Endrick aliingia dakika ya 61, magoli mengine ya Brazil yamefungwa na Andrea Pereira na Gabriel Martinelli.