Eng. amaliza kazi, nyota Mazembe, Saint Eloi Lupopo watua Yanga
Eric Buyanza
May 16, 2024
Share :
Habari zilizotufikia zinasema tayari Klabu ya Yanga chini ya uongozi wa Eng Hersi imefanikiwa kuwanasa nyota wawili kutoka Jamhuri ya Kongo.
Imeelezwa kuwa nyota hao ni beki Chadrack Issaka Boka aliyetoka Saint Eloi Lupopo na winga wa kulia Beni Phillipe Kinzumbi kutoka klabu tajiri nchini humo, TP Mazembe.
Habari za ndani kabisa zinasema wachezaji hao tayari wameshaingia mikataba ya kuitumikia klabu hiyo kongwe nchini yenye maskani ya kudumu Jangwani jijini Dar es salaam.
Chadrack huenda akachukua nafasi ya Joyce Lomalisa ambaye mkataba wake unakaribia kutamatika mwishoni mwa msimu huu.