Eng. Hersi aelezea hatua zilizobaki 'Transformation' Yanga
Sisti Herman
April 1, 2024
Share :
Uongozi wa Yanga chini ya Eng. Hersi Said umesema kuwa umebakiza hatua mbili katika kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo 'Transformation'.
Hatua hizo mbili kufanya tathmini ya kipi ambacho klabu hiyo itachangia katika kampuni itakayoundwa kuiendesha Yanga na ya pili ni kuunda kampuni yenyewe.
"Cha kwanza ambacho tunaenda kufanyani kufanya tathmini ya kujua klabu yetu ina thamani gani. Eneo la pili ili kampuni hii ifunguliwe ni lazima kuwe na 'Capital Contribution' (uchangiaji wa mtaji).
"Jukumu la tatu ni kuruhusu utaratibu wa usawa utakauruhusu mauzo ya zile asilimia 49 ambazo zitakuwa zinajenga ile kampuni hiyo ndio hatua inayofuata usoni kwetu na baada ya hapo kuijenga hiyo kampuni," alisema Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said.