Eng. Hersi aongoza EXCOM ya kwanza Yanga 2024
Sisti Herman
January 29, 2024
Share :
Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga chini ya Rais wetu Eng.Hersi Ally Said jana tarehe 28.01.2024 wamekaa kikao cha kwanza cha kikatiba kwa mwaka 2024 katika ukumbi wa mikutano Best Western Hoteli, jijini Dodoma.
Kikao hicho pamoja na ajenda nyingine kilijikita zaidi katika mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji ambayo yataendelea mwaka huu pamoja na maendeleo ya idara mbalimbali za Klabu hiyo.