Eng. Hersi kuwavalisha Simba medali za CAF
Sisti Herman
April 29, 2025
Share :
Kwa kawaida kwenye mechi za Fainali za CAF zoezi la kuwavalisha medali wanafainali wa michuano ya CAF, kama Ligi ya Mabingwa Afrika, kombe la shirlikisho viongozi waandamizi wa shirikisho hilo kama Rais wa CAF, Rais wa Shirikisho la nchi na viongozi wengine.
Tangu mwaka 2023, CAF wametangaza kuanzisha taasisi itakayokuwa inasimamia vilabu ACA, ambayo Rais wake kwasasa ni Mtanzania Hersi Said Ally, Rais wa klabu ya Yanga.
Kuna uwezekano mkubwa sana Rais wa ACA, Eng. Hersi Said ambaye ni Rais wa Yanga akashiriki zoezi la kuwavalisha medali wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa watani zake Simba ambao wamefika fainali za michuano hiyo.
Simba wana uhakika wa kuvaa medali, haijalishi wakiwa mabingwa au wasipokuwa mabingwa.