England yaitandika Hispania ugenini
Sisti Herman
November 15, 2026
Share :

Rekodi ya Uhispania ya kutofungwa kwa miaka miwili na nusu imefika mwisho baada ya mabingwa hao wa dunia kufungwa mabao 3-2 na timu ya Taifa Uingereza.
Mara ya mwisho kwa Uhispania kupoteza mchezo ilikuwa mwezi Machi 2024.
Hata baada ya kubaki na wachezaji 10 uwanjani na kuruhusu mabao mawili yaliyofungwa na Mikel Oyazerbal na Nico Williams, waliendelea 'kushikilia bomba'.
Magoli ya Uingereza kwenye mchezo huu yamefungwa na Harry Kane, Ezri Konsa na Ben White.





