pmbet

England yashindwa kutamba tena nyumbani, Mainoo akitwaa tuzo

Sisti Herman

March 27, 2024
Share :

Timu ya Taifa ya Uingereza jana imeshindwa tena kutamba kwenye dimba lao la nyumbani Wembley baada ya kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Ubelgiji kwenye mchezo wa kimataifa wa Kalenda ya FIFA wakijiandaa na michuano ya Euro 2024.

England ambao walisawazisha dakika za jioni mabao yao yalifungwa na mshambuliaji wa Brendford Ivan Toney na kiungo mshambuliaji wa Real Madrid Jude Bellingham ambaye alisawazisha magoli mawili ya Ubelgiji yaliyofungwa na kiungo mshambuliaji wa Aston Villa Youri Tielesman.

Mchezo huo pia ulishuhudia kinda wa Manchester United akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo wa Uingereza ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Uingereza imeshindwa kutamba nyumbani kwenye mchezo huo wa pili mfululizo baada ya mchezo kabla ya huo kufungwa 1-0 na Brazil.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet