pmbet

Enoch Sontonga, raia wa Afrika Kusini aliyebuni wimbo wetu wa Taifa

Eric Buyanza

July 20, 2024
Share :

Huyu ni Enoch Sontonga, raia wa Afrika Kusini, aliyekuwa mwalimu wa shule ya misheni ya Methodisti, ndiye aliyebuni wimbo wa ‘Mungu Ibariki Afrika’ ambao kwa lugha ya Afrika Kusini unajulikana kama ‘Nkosi Sikelel’ iAfrika’. 

Mungu Ibariki Afrika ni jina la Wimbo wa Taifa wa Tanzania ambao asili yake ni Wimbo wa Nkosi Sikelel’ i Afrika wa Afrika Kusini. 

Sehemu ya wimbo huu inatumika pia katika nyimbo za Zambia na huko nyuma ulitumiwa pia kama Wimbo wa Taifa wa Zimbabwe.

Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki Aprili 18, 1905 na alitokea Eastern Cape Province, Jimbo la Wakosa (Xhosa), ambako pia ni nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa taifa hilo Nelson Mandela. 

Alitunga wimbo huo mwaka wa 1897 kwa lugha yake ya Kikosa na ulikuwa wimbo maarufu sana kanisani mpaka pale ulipokuja kukubaliwa na kuanza kutumika kwenye mikutano ya kisiasa.

Wimbo huo siyo wa watu wa Afrika Kusini tu kwani Sontonga aliandika na kutunga wimbo huo kama wimbo wa bara lote. 

Ndiyo maana alisema Nkosi Sikelel’ iAfrika, yaani God Bless Africa na siyo God Bless South Africa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet