pmbet

Enzo aingia kwenye rada za Atletico

Sisti Herman

April 1, 2025
Share :

 

Atletico Madrid inahitaji saini ya kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Argentina, Enzo Fernandez katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza Atletico inataka kutoa Pauni 25 milioni pamoja na kiungo wao Pablo Barrios kama sehemu ya ofa ya staa huyo.

Hata hivyo, ofa hiyo inaonekana kuwa ndogo sana kiasi kuishawishi Chelsea imuuze fundi huyo iliyemnunua kwa zaidi ya Euro 100 milioni.

Inaelezwa, Atletico inamtumia pia, Julian Alvarez kama sehemu ya ushawishi kwa sababu yupo karibu sana na kiungo huyo.

Tangu msimu huu uanze, Enzo ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2032, amecheza mechi 35 za michuano yote na kufunga mabao matano.

Enzo alianza msimu kwa kusuasua pale Chelsea lakini hatimaye alibadili upepo na kucheza kwa kiwango bora hadi akiwa na Argentina.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet