Enzo Maresca kubebeshwa mikoba ya Guardiola Man City
Eric Buyanza
May 19, 2026
Share :

Enzo Maresca anatarajiwa kuchukua mikoba ya Pep Guardiola kama kocha wa Manchester City kabla ya msimu ujao, huku taarifa zikidodosa kuwa mazungumzo yako katika hatua nzuri.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 46 anatarajiwa kutangazwa rasmi kuwa mrithi wa Guardiola muda utakapowadia.
Itakumbukwa kuwa Maresca alikuwa msaidizi wa Guardiola wakati Man City iliposhinda mataji matatu msimu wa 2022-23.





