Euro milioni 30 tu! Kumletea Arteta winga kutoka Girona
Eric Buyanza
June 5, 2024
Share :
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anatamani huduma ya winga wa Ukraine Viktor Tsygankov.
Winga huyo wa klabu ya Girona, ameonyesha ushawishi mkubwa kwa mabosi wa Arsenal, na inaaminika anaweza kupatikana kwa gharama ya Euro milioni 30 tu.
Tsyganov mwenye umri wa miaka 26, amechochea sehemu kubwa ya mafanikio ya klabu ya Girona chini ya meneja Michel Sanchez kwa kufanikiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia klabu hiyo.