Evra ataka Luis Enrique apewe mikoba Man Utd
Eric Buyanza
March 10, 2026
Share :
Beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amempendekeza Luis Enrique, kocha wa Paris Saint-Germain, kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.
Evra anasema Enrique ana falsafa ya soka inayolingana na mahitaji ya Manchester United, na kwamba anaweza kuleta nidhamu na ari kwa wachezaji.
Evra alisifia uwezo wa Enrique wa kuiongoza timu yake ya zamani, Barcelona, na sasa PSG, kusaka kombe la UEFA Champions League.
Aliongeza kuwa wachezaji wa Manchester United watahitaji kufanya kazi kwa bidii kubwa chini ya Enrique.






