Ewura yatangaza bei mpya ya Mafuta, Petroli Dsm kuuzwa 3,314
Eric Buyanza
May 1, 2024
Share :
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za bidhaa za mafuta ya petrol, zitakazo anza kutumika kuanzia leo hii , Jumatano tarehe 1 May 2024.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo bei kwa mkoa wa Dar es salaam Petroli itauzwa shilingi 3,314 huku Dizeli ikiuzwa 3,196.