pmbet

FAGIO LA CHUMA KUPITA ARSENAL: Wafanyakazi 60 kupoteza ajira

Eric Buyanza

October 17, 2026
Share :

Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta, amethibitisha kuwa ameelezwa na uongozi wa juu wa klabu hiyo kuwa uamuzi wa kupunguza wafanyakazi utasaidia timu hiyo kuendelea kupiga hatua na ‘kufikia mafanikio’ makubwa zaidi katika siku zijazo.

 

Kauli hiyo inakuja kufuatia ripoti zilizovuja kuwa klabu hiyo inajiandaa kuachana na takriban wafanyakazi 60, ambao ni sawa na asilimia 7 ya nguvu kazi yake ya kudumu, kufuatia tathmini ya kina ya kiuendeshaji iliyofanywa na kampuni ya nje chini ya Mtendaji Mkuu, Richard Garlick.

 

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Nottingham Forest, Arteta alikiri kufanya kikao na mabosi wa klabu hiyo ambapo walimfafanulia sababu za kiuchumi na kimkakati zilizopelekea kufikia hatua hiyo ngumu.

 

"Nilielezwa kuhusu zoezi hilo na uchambuzi uliofanywa klabuni, kukiwa na nia ya kuendelea kukua na kuboresha mambo," alisema Arteta. "Baadhi ya maamuzi lazima yachukuliwe ili kuweka watu kwenye nafasi sahihi na kuendelea kuwekeza ili kufikia yale tunayotaka kufikia na mafanikio tunayotaka kuyatengeneza."

 

Hata hivyo, kocha huyo raia wa Uhispania alisisitiza kuwa yeye si mtu sahihi wa kuzungumzia masuala ya biashara na muundo wa utawala wa klabu hiyo, kwani majukumu yake makuu yanabaki uwanjani.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet