pmbet

Fainali klabu bingwa ya ngumi kufanyika leo Tanga

Eric Buyanza

August 28, 2026
Share :

Fainali za Mashindano ya Ngumi ya Klabu Bingwa ya Taifa Tanga 2026 zinatarajiwa kufanyika leo jioni katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Mjini, huku jumla ya mapambano 13 yakitarajiwa kupigwa.

 

Mashindano hayo yaliyoanza Jumanne, tarehe 25 Agosti 2026, yamefikia kilele huku jumla ya mabondia 26 wakitarajiwa kushuka ulingoni katika mapambano 13 ya fainali.

 

Mabingwa watetezi, Ngome, wanaongoza kwa kuwa na mabondia tisa waliofuzu fainali, wakifuatiwa na MMJKT yenye mabondia sita na Magereza yenye mabondia wanne.

 

JKT Mgulani imeingiza mabondia watatu, huku General Chande ya Tanga, Band Coy na Mashujaa zikiwa zimeingiza bondia mmoja mmoja katika fainali hizo.
Miongoni mwa mapambano yanayosubiriwa kwa hamu ni la uzani wa Light Heavyweight (80kg), litakalowakutanisha Eliankunda Daniel wa MMJKT na Enzi Kasililika wa Magereza.

 

Mabondia hao watakutana kwa mara nyingine baada ya kukabiliana katika fainali za Mashindano ya Taifa ya Ubingwa wa Wazi yaliyofanyika Dar es Salaam mwezi Aprili 2026, ambapo Eliankunda aliibuka mshindi kwa pointi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet