"Fainali tumewanyamazisha wengi fainali aje yeyote"-Cubarsi.
Joyce Shedrack
July 15, 2026
Share :
Beki wa Hispania, Pau Cubarsí, amesema anamtaka mpinzani yeyote kwenye fainali ya Kombe la Dunia iwe ni Argentina au Uingereza huku akiweka wazi wamefanikiwa kuwafunga watu midomo kuhusu safu yao ya uinzi.

Akizungumza baada ya Hispania kutinga fainali, Cubarsí amesema “Nataka nani kwenye fainali, Argentina au Uingereza? Aje yeyote. Sina upendeleo kwa timu yoyote, na iwe jinsi Mungu atakavyopenda. Sasa tutapumzika na kurejesha nguvu. Kesho tuna safari ndefu kuelekea New York, kisha tutaanza kumchambua mpinzani wetu.”
“Kulikuwa na maneno kwamba safu yetu ya ulinzi na makipa hawakuwa kwenye kiwango bora, lakini naamini tumewanyamazisha wengi.”
Beki huyo alisifu mshikamano wa kikosi kizima baada ya kufanikiwa kuruhusu bao moja pekee hadi kufika fainali.
“Tumefungwa bao moja tu na tumefika fainali. Nafikiri tunafanya kazi nzuri sana, na mafanikio haya yanatokana na kila mmoja wetu, wanaocheza na waliopo benchi. Kiwango wanachoonyesha mazoezini kinamsaidia kila mchezaji kuwa bora zaidi.”





