Fainali ya 'FA' sasa kupigwa Zanzibar, siyo Babati tena
Sisti Herman
May 22, 2024
Share :
Fainali ya kombe la shirikisho la TFF (CRDB Federation Cup) iliyopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati sasa imehamishwa uwanja na itachezwa kwenye dimba la New Amaan, Zanzibar.
Uuamuzi huo umefanywa na kamati ya Utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu (TFF) baada ya baadhi ya miundombinu muhimu mjini Babati kutokuwa tayari kwaajili ya fainali hiyo pamoja na sababu za kiusalama.
Fainali hiyo itakayozihusisha klabu za Yanga na Azam itachezwa kwenye dimba la Amaan kuanzia saa 2:15 usiku.