Fainali za kombe la dunia ni Spain vs Brazil - Neymar
Eric Buyanza
June 23, 2026
Share :

Nyota wa Brazil, Neymar amezipuuza Argentina ya Lionel Messi na Ureno ya Cristiano Ronaldo alipoulizwa kuhusu timu ambayo angependelea kukutana nayo katika fainali ya Kombe la Dunia la 2026.
Brazil imebakiza mechi moja ya hatua ya makundi dhidi ya Scotland, kufuatia ushindi na sare.
Fowadi huyo wa klabu ya Santos hajacheza mechi yoyote ya kombe la dunia akikosa michezo miwili ya kwanza ya hatua ya makundi kutokana na jeraha.
Alirejea mazoezini na timu wiki iliyopita na huenda akacheza mechi ijayo dhidi ya Scotland mnamo Juni 24.
Akiongea na mtandao wa kijamii wa Puma Football, Neymar aliulizwa kuhusu timu gani angependa kukutana nayo kwenye fainali na akajibu;
"Hispania. Brazil vs Hispania."





