Fair Play: Edna Lema ampongeza Mgosi kwa kushinda Dabi ya Kariakoo
Sisti Herman
May 17, 2026
Share :

Baada ya juzi Simba Queens kushinda 2-1 kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga Princess, kocha mkuu wa Yanga Princess Edna Lema 'Mourinho' ameonyesha uungwana wa kiushindani kwa kumpongeza kocha wa Simba Queens Mussa Hassan 'Mgosi'.
Kupitia Instagram yake Edna Lema aliandika "Pamoja na itikadi za timu zetu lakini sisi ni vijana tunaopambana kutafuta rizki kwaajili ya maisha ya familia zetu, hongera kwa kushinda dabi kocha kijana Mussa Mgosi"
Edna ameandika hivyo baada ya Simba Queens kushinda mchezo huo wa Ligi kuu wanawake uliochezwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.





