pmbet

Familia yaridhia Mwili wa Mkenya aliyefariki Mlima Everest kuachwa mlimani

Sisti Herman

May 30, 2024
Share :

Familia ya Mpanda Milima, Joshua Cheruiyot Kirui, aliyefariki wakati akipanda Mlima Everest Mei 22, 2024, imesema Mwili huo utaachwa alikofia kutokana na gharama na hatari za mchakato wa kuurejesha mwili wake nchini humo

Cheruiyot alianguka kwenye Ufa uliopo umbali wa Mita 48 kutoka kwenye Kilele cha mlima huo wenye Mita 8,848.86 ambapo imeelezwa kuurejesha mwili wake kutoka umbali huo itakuwa ni hatari kwa timu ya uokoaji, na familia haipo tayari kuhatarisha maisha ya wengine

Inakadiriwa kuwa karibu miili 200 kati ya wapandaji 330 waliofariki kwenye mlima Everest ambao ndio mrefu zaidi duniani, bado ipo katika eneo hilo

Inaelezwa kuwa gharama za kuurejesha mwili ni Ksh. Milioni 9 (takriban Tsh. Milioni 178) na itahitaji Watu 8 kupanda juu na kubeba mwili huo. Kutokana na hilo, Familia nyingi zinazopoteza wapendwa wao huamua kuwaacha huko.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet