Farid apewa miaka miwili Yanga
Sisti Herman
July 2, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imemuongezea mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Farid Mussa kwa miaka miwili zaidi.
Farid ambaye aliunga na Yanga mwaka 2020 akitokea CD Tenerrife B ya Hispania na amedumu kwa misimu minne mfululizo Yanga hadi sasa.
Kabla ya kwenda Ulaya Farid alikuwa mchezaji wa klabu ya Azam kuanzia timu za vijana.