Faru weusi wapaa Scotland kushiriki michezo ya madola 2026
Eric Buyanza
July 22, 2026
Share :

Timu ya Taifa ya Ngumi, maarufu kama Faru Weusi , jana usiku iliondoka nchini kuelekea Glasgow, Scotland kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola 2026.
Faru Weusi itawakilishwa na nahodha Yusufu Changalawe (80kg – Light Heavyweight), Faki Issa Faki (55kg – Bantamweight) na Zawadi Kutaka, chini ya uongozi wa Mwalimu Mkuu Samwel Kapungu "Batman".
Katika msafara huo, timu ya ngumi iliambatana na Timu ya Taifa ya Kuogelea, inayoundwa na muogeleaji Collins Saliboko pamoja na kocha wake Kanisi Mabena.
Sherehe rasmi za ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola Glasgow 2026 zinatarajiwa kufanyika tarehe 23 Julai 2026 jijini Glasgow, Scotland. Tanzania itawakilishwa na jumla ya wanamichezo 12 kutoka michezo ya Ngumi (3), Riadha (6), Judo (2) na Kuogelea (1).





