pmbet

Fatma Karume; Chadema haiwezi kuzuia uchaguzi

Sisti Herman

July 7, 2025
Share :

 

Mwanaharakati Fatma Karume amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo hakioni kikiweza kuzuia uchaguzi kwa mwaka huu wa 2025 huku akieleza kuwa kufanya hivyo ni kufanya jinai.

Kupitia mtandao wa X Fatma aliulizwa na mdau kama atashiriki kupiga kura akasema atashiriki kwa sababu yeye ni haki yake huku akieleza kuwa mwaka 2016 chama cha CUF na ACT Wazalendo waliposusia uchaguzi wa marudio kule Zanzibar viliathirika sana na yeye alivikosoa kwa kufanya hivyo.

“Wanaonielewa na wanaonisoma wanajua siamini kuwa muarubaini wa mfumo mbovu wa Uchaguzi ni kususia uchaguzi.”

Fatma ameongeza kuwa ni muhimu uwepo wa maoni ya vyama pinzani katika bunge ili kusaidia kuboresha utungwaji wa sheria ambazo ni bora zaidi katika taifa.

“Maoni pinzani ni muhimu sana na lazima yawepo Bungeni.”

“no reform no election Inaweza kufanya kazi kama CDM(CHADEMA) wana uungwaji mkono wa kutosha ngazi ya chini (grassroots).”

Pamoja na kukubali kuwa kuna umuhimu wa kufanyika kwa maboresho kwenye sheria na mifumo ya uchagu Fatma amesema kwa sasa CHADEMA haina uungwaji mkono wa kutosha kuweza kuzuia uchaguzi hivyo ni wakati mzuri kwao kukaa na kukubaliana(negotiate).

“Lakini CDM(CHADEMA) hawana idadi ya kutosha kulazimisha mageuzi kwa kuvuruga uchaguzi. CDM wanahitaji kufanya mazungumzo (negotiate)” amesema Fatma

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet