Faye: Afrka inaweza kulisha dunia nzima
Sisti Herman
September 2, 2025
Share :
Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, siku ya Jumatatu alisema kuwa Afrika inaweza kulisha dunia nzima, akisisitiza kuwa vijana lazima wawe kiini cha mageuzi ya kilimo.
Rais Faye aliyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wa usalama wa chakula uliofanyika Dakar nchini Senegal na kuongeza kuwa, asilimia 65 ya ardhi inayofaa kwa kilimo duniani, na vijana wabunifu, na rasilimali nyingi ziko barani Afrika.
Rais Faye alihimiza Afrika ijiegemee yenyewe kufanikisha usalama wa chakula na kuchukua mtazamo wa kutafuta suluhisho, akisema hilo linahitaji uwekezaji mkubwa katika usimamizi wa maji, ubunifu, usindikaji wa mazao ndani ya nchi, na biashara kati ya nchi za Afrika.