pmbet

Fedha za maadhimisho ya Uhuru kutumika kutoa huduma za kijamii.

Joyce Shedrack

December 4, 2024
Share :

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa mwaka 2024 yafanyike katika ngazi ya mikoa na fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zitumike katika kutoa huduma za kijamii.

Waziri Mkuu ametoa maagizo kuwa kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira katika maeneo ya kijamii kama vile kwenye masoko, hospitali, kambi za wazee na wenye mahitaji maalum, mashindano ya michezo mbalimbali pamoja na makongamano na midahalo ya kujadili maendeleo endelevu ambayo nchi yetu imefikia katika kipindi cha miaka 63 ya Uhuru ifikapo hiyo tarehe 9 disemba mwaka huu.

 

“Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa”.

Mheshimiwa Majaliwa amesema hayo leo Jumatano, Disemba 4, 2024 katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet