Fei aifikisha Azam Kileleni
Sisti Herman
March 7, 2024
Share :
Klabu ya Azam imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Coastal ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Semkufo Charles dakika ya 68 kabla ya Azam kusawazisha kupitia nyota wa kikosi hicho, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na kuisaidia Azam kupanda juu kwenye msimamo wa ligi baada ya mchezo wake wa 20 msimu huu na kuishusha Yanga hadi nafasi ya pili na pointi 43 ingawa imecheza michezo 16.
Bao la Feisal linamfanya kuendelea kuongoza kwenye mbio za ufungaji akifikisha mabao 12, nyuma ya Stephane Aziz KI wa Yanga mwenye 10 huku kwa upande wa Semkufo Charles akiendelea kufanya vizuri na kikosi hicho baada ya kufikisha mabao manne.