Fei hakamatiki huko, aongoza kwa magoli, Azam ikiiua Dodoma
Sisti Herman
March 3, 2024
Share :
Baada ya ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Dodoma Jiji huku yeye akifunga mabao mawili, kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum sasa anaongoza mbio za ufungaji wa mabao kwa kufikisha mabao 11 na kumpiku kiungo wa Yanga Stephanie Aziz Ki kwenye nafasi ya kwanza.
Mabao mengine ya Azam yamefungwa na Ayoub Lyanga na Kipre Jr na kuisaidia Azam kupanda hadi nafasi ya pili nyuma ya Yanga huku wakiwa na idadi kubwa ya michezo zaidi ya Simba waliopo nafasi ya 3.