Fei Toto amuonya Shekhan
Eric Buyanza
December 19, 2023
Share :
Mchezaji wa zamani wa Yanga, Feisal Salum Abdallah a.k.a Feitoto a.ka Zanzibar Finest, ametoa maoni yake kwa kuhusu usajili wa Yanga wa mchezaji wa Shekhan Ibrahim.
Feisal anasema kwamba Shekhan Ibrahim ni Bonge la mchezaji mwenye kipaji na uwezo mkubwa sana, lakini pia akamuonya mapema kwa kumtaka ajipange kwelikweli kwasababu ametua kenye timu yenye pressure kubwa.
"Shekhan ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na ana kipaji....namuona mbali natarajia atafanya vizuri akipewa nafasi na atapata mafanikio makubwa ndani ya timu yake....najua amekuja timu kubwa anataka kupambana na kuonesha kile alichonacho bila kujali anaenda kupambana na mastar gani"
Akiendelea Feisal amesema....."Ni mchezaji ambaye nimemshuhudia ni mdogo wangu ameanza kujulikana sasa lakini pia ni mchezaji amekuzwa na kuwa bora chini ya JKU, amepita kwenye misingi ya soka hivyo naamini atakuwa bora katika kipindi hiki ambacho anacheza katika kikosi cha Yanga" alimalizia Feitoto.