Feisal na Aziz Ki kwenye vita kiatu cha dhahabu
Sisti Herman
April 15, 2024
Share :
Wakati ligi kuu Tanzania bara ikielekea ukingoni, mbali na vita ya Ubingwa ambayo ipo mikononi mwa vilabu vya Yanga, Simba na Azam kwenye nafasi tatu za juu, vita nyingine kubwa ni ile ya kuwania kiatu cha dhahabu ambayo huhusisha wachezaji wanaoongoza kwa idadi kubwa ya upachikaji wa magoli ambapo kwasasa imetawaliwa na wachezaji wawili, Feisal Salum wa Azam na Stephanie Aziz Ki wa Yanga.
Kwenye orodha ya wananoongoza kwa mabao mengi hadi sasa, Aziz Ki anaoongoza akiwa na mabao 14 huku akifuatiwa na Feisal mwenye mabao 13 huku kila mmoja akiwa na mwendelezo wa kiwango bora msimu huu.
Wachezaji hao mbali na kazi hiyo ya ziada kwao, kwani ni viungo washambuliaji wenye majukumu ya kupika zaidi mabao kuliko kufunga, kwenye majukumu yao mama hadi sasa kila mmoja amefanya vyema ambapo Aziz Ki amepika mabao 7 huku Fei akipika mabao 6.
Je nani atabeba kiatu cha dhahabu msimu huu?