Feitoto aiua Ihefu, kimyakimya anakitaka kiatu cha dhahabu
Sisti Herman
April 22, 2024
Share :
Baada ya siku ya jumamosi kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki kufunga bao moja kwenye dabi ya Kariakoo wakishinda 2-0 na kuongeza magoli ulimfanya aongoze orodha ya wafungaji bora hadi sasa akifikisha goli 15, kiungo wa klabu ya Azam ambaye anamkimbiza Aziz kwenye mbio hizo naye amekataa unyonge baada ya jana kufunga dhidi ya Ihefu.
Kwenye ushindi huo wa 1-0, Feisal aliendelea kuwa Mwokozi wa matokeo wa Azam baada ya kufunga bao hilo la pekee ambalo limemfanya kufikisha mabao 14 na kushika nafasi ya pili kwenye vita ya kuwania kiatu cha dhahabu.
Je Feitoto anaweza kutwaa kiatu cha dhahabu?